Hamia kwenye habari

JULAI 12, 2018
JAPANI

Mafuriko Yaharibu Vitu Mashariki mwa Japani

Mafuriko Yaharibu Vitu Mashariki mwa Japani

Watu 169 wameuawa mashariki ya Japani, na familia zaidi ya 255,000 bado hazina maji baada ya mvua kubwa kunyesha zilizosababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi.

Ingawa hakuna Shahidi wa Yehova aliyekufa, ndugu 200 walihamishwa na dada mmoja alijeruhiwa. Dada aliyejeruhiwa alitibiwa hospitalini na sasa anapata nafuu. Nyumba 103 hivi za ndugu zetu zimeharibiwa kwa kiasi fulani, na moja imeharibiwa kabisa. Pia Majumba 11 ya Ufalme na Jumba la Kusanyiko yameharibiwa kwa kiasi fulani na mafuriko.

Halmashauri nne za Kutoa Misaada (DRC) zimepangwa ili kuwafariji na kuwatia moyo ndugu na dada walioathiriwa kupitia Maandiko na kutoa msaada, kama vile wa chakula, mavazi, na maji safi. Halmashauri hizo pia zitapanga msaada wa kudumu, kama vile kusafisha, kuua viini au wadudu, na kurekebisha nyumba zilizoharibiwa za ndugu zetu.

Tunasali kwa ajili ya ndugu na dada zetu walioathiriwa na majanga haya nchini Japani na tunatazamia kwa hamu wakati ambapo Yesu atatumia nguvu zake kuondoa majanga milele.—Mathayo 8:26, 27.