Hamia kwenye habari

JUNI 5, 2019
AFRIKA KUSINI

Afrika Kusini Yakabiliana na Mvua Kubwa na Mafuriko

Afrika Kusini Yakabiliana na Mvua Kubwa na Mafuriko

Mvua kubwa zilipiga pwani ya Afrika Kusini mwishoni mwa Aprili 2019. Mvua zilizoendelea kwa muda mrefu zilisababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi katika eneo la Durban, mkoa wa KwaZulu-Natal na maeneo yaliyo karibu. Ripoti zilizotufikia zinaonyesha kwamba watu 70 hivi wamekufa.

Ofisi ya tawi ya Afrika Kusini inaripoti kwamba hakuna ndugu au dada waliojeruhiwa au kuuawa. Hata hivyo, nyumba za familia 19 ziliharibiwa na maporomoko au mafuriko. Mafuriko pia yaliharibu Majumba ya Ufalme matatu hivi.

Chini ya mwongozo wa Halmashauri ya Kutoa Misaada, wajitoleaji wa Idara ya Usanifu-Majengo na Ujenzi wanakagua kiwango cha uharibifu kwa kila nyumba iliyoathiriwa. Katika hali ambazo usalama wa akina ndugu umehatarishwa, mipango inafanywa ili kuwatafutia makao maeneo mengine.

Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kuwategemeza ndugu na dada zetu nchini Afrika Kusini wanaposhughulikia hali hiyo ngumu.—Zaburi 34:19.