Hamia kwenye habari

Ofisi mpya ya utafsiri ya Lugha ya Ishara ya Afrika Kusini

APRILI 29, 2022
AFRIKA KUSINI

Idara ya Usanifu-Majengo na Ujenzi Yakarabati Ofisi ya Utafsiri ya Lugha ya Ishara ya Afrika Kusini

Idara ya Usanifu-Majengo na Ujenzi Yakarabati Ofisi ya Utafsiri ya Lugha ya Ishara ya Afrika Kusini

Hivi karibuni, Idara ya Usanifu-Majengo na Ujenzi (LDC) nchini Afrika Kusini, itakamilisha ukarabati wa jengo la ofisi mjini Durban ambalo litatumika likiwa ofisi ya utafsiri (RTO) ya Lugha ya Ishara ya Afrika Kusini (SASL). Ofisi ya tawi ilinunua jengo hilo Machi 2020 na baada ya muda mfupi ikanunua nyumba kadhaa zilizokuwa karibu na jengo hilo. Watafsiri wataanza kuhamia kwenye nyumba hizo Mei 2022.

Kuna Wanabetheli 17 na wajitoleaji 25 wa muda wanaofanya kazi mbalimbali za ofisi ya utafsiri. Ofisi hiyo imejengwa kwenye eneo linalofaa na hilo litawasaidia watafsiri kuandaa machapisho yenye ubora kwa ajili ya wahubiri 283 ambao ni viziwi na walio na matatizo ya kusikia nchini Afrika Kusini. Machapisho hayo yatawasaidia pia watu 450,000 ambao ni viziwi na walio na matatizo ya kusikia nchini humo. Idadi kubwa ya viziwi na watu walio na matatizo ya kusikia nchini Afrika Kusini wanaishi kwenye jimbo la KwaZulu-Natal. Durban ndio mji mkubwa zaidi kwenye jimbo hilo.

Ndugu Sibusiso Mzizi, anayefanya kazi katika kikundi cha utafsiri cha Lugha ya Ishara ya Afrika Kusini anasema hivi: “Tunaamini kwamba ofisi hii mpya itakuwa msaada mkubwa sana kwa eneo la Lugha ya Ishara nchini Afrika Kusini na pia kuyaimarisha makutaniko.”

Tunamshukuru sana Yehova kwa kubariki jitihada zetu katika Lugha ya Alama (SASL) na pia kuufanya mradi huu uendelee.​—Zaburi 127:1.