SEPTEMBA 16, 2019
AFRIKA KUSINI
Johannesburg, Afrika Kusini—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”
Tarehe: Septemba 6-8, 2019
Mahali: Uwanja wa Michezo wa FNB Johannesburg, Afrika Kusini
Lugha za Programu: Kiingereza, Kisesotho, Kizulu
Idadi ya Wahudhuriaji: 58,149
Idadi ya Waliobatizwa: 476
Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 6,000
Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Bolivia, Congo (Kinshasa), Finland, Hong Kong, Hungaria, Israel, Japani, Kenya, Korea, Liberia, Madagaska, Malawi, Marekani, Paraguai, Peru, Uganda, Uingereza, Ulaya ya Kati, Zambia, Zimbabwe
Mambo Yaliyoonwa: Wasimamizi wa hifadhi ambayo wajumbe walitembelea inayoitwa Lion and Safari Park, walieleza kwamba hawajawahi kuona watu wa utamaduni na lugha nyingi tofauti-tofauti kadiri hiyo wakishuka kutoka kwenye basi moja bila ubishi au malalamiko. Wasimamizi hao walivutiwa sana na jinsi wageni walivyofuata mwelekezo na kushirikiana na wafanyakazi hivi kwamba wakasema: “Tulifurahi sana kwamba walitutembelea!”
Kikundi cha ndugu na dada wenyeji kwenye uwanja wa ndege wakiwakaribisha wajumbe waliowasili nchini Afrika Kusini
Akina dada wanne, wawili wenyeji na wajumbe wawili, wakisambaza mialiko ya kusanyiko katika huduma
Wahudhuriaji wa kusanyiko wakiwa wamevaa mavazi ya kitamaduni wakisimama ili kupigwa picha
Ndugu na dada wakitabasamu na kupiga makofi wakati wa kusanyiko
Mmoja kati ya watu 476 waliobatizwa
Ndugu Anthony Morris, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akiwasalimu akina ndugu na dada wakati wa mapumziko
Watumishi wa wakati wote kutoka nchi nyingine wakitambulishwa mbele ya wahudhuriaji, siku ya mwisho ya kusanyiko
Picha ya akina dada watatu baada ya programu ya kusanyiko
Kwaya iliyovalia mavazi yenye kupendeza ya Kiafrika ikiwatumbuiza wasikilizaji wakati wa tafrija ya jioni