Hamia kwenye habari

AGOSTI 29, 2017
ANGOLA

Mashahidi Katika Kusanyiko Nchini Angola Walemewa na Gesi Yenye Sumu

Mashahidi Katika Kusanyiko Nchini Angola Walemewa na Gesi Yenye Sumu

Asubuhi ya Ijumaa, Agosti 25, 2017, wakati wa kusanyiko lililofanywa katika Jumba la Kusanyiko la Viana huko Luanda, Angola, wahudhuriaji 405 walipoteza fahamu wakati wavamizi walipowapulizia gesi yenye sumu katika jumba kuu na vyooni. Inafurahisha kwamba gesi hiyo haikuwa hatari na hakuna aliyekufa. Walioathiriwa walipelekwa hospitalini na wengi wao walitibiwa na kuruhusiwa warudi nyumbani ndani ya saa chache. Uchunguzi unafanywa na wenye mamlaka; wanaume watatu walikamatwa na kupelekwa kwenye kituo cha polisi Ijumaa mchana.

Ofisi ya tawi ya Luanda imesema kwamba wote walioathiriwa wanapata nafuu. Wale waliohudhuria kusanyiko hawakushtuka kupita kiasi na walifanya kazi pamoja kuwasaidia walioumia. Kwa sababu ya mapendekezo ya polisi, kipindi cha kusanyiko cha Ijumaa alasiri kiliahirishwa. Hata hivyo, Jumamosi, Agosti 26, na Jumapili, Agosti 27 kusanyiko liliendelea bila matatizo. Hudhurio lilifikia watu zaidi ya 12,000, na 188 walibatizwa na kuwa Mashahidi wa Yehova.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000

Angola: Todd Peckham, +244-923-166-760