FEBRUARI 2, 2022
ARGENTINA
Familia ya Betheli Inafurahia Makao Mapya Nchini Argentina
Familia ya Betheli nchini Argentina imehamia katika majengo mapya ya ofisi ya tawi. Mwanakandarasi kutoka nje alikamilisha ujenzi katika majira ya kiangazi ya 2021. Tangu wakati huo, Wanabetheli na wajitoleaji wa ujenzi wanaendelea kumalizia kazi ndani ya majengo hayo mapya. Kwa mfano, wamekuwa wakiunganisha vifaa vya mbao, kufanya usafi mkubwa, kuunganisha mabomba, na kazi za umeme.
Ofisi hiyo inatia ndani jengo la ofisi lililo na maeneo 136 ya kufanyia kazi na majengo mawili ya makazi yaliyo na vyumba 98. Ofisi ya tawi ya awali ilifanyizwa na majengo kadhaa yaliyokuwa katika maeneo mbalimbali. Ofisi mpya ya tawi inawawezesha Wanabetheli kuishi na kufanya kazi kwenye jengo moja. Eneo hilo lina jumla ya mita 8,524 za mraba na liko nje ya Buenos Aires, mji mkuu wa Argentina.
Ndugu Humberto Cairo, mshiriki wa Halmashauri ya Tawi anasema hivi: “Yehova ameonyesha ukarimu wake mwingi wakati wa mradi huu. Majengo haya mapya yanang’aa hasa kwa sababu ya nembo ya jw.org inayotambulika kwa urahisi.”
Ndugu Sebastian Rosso, anayefanya kazi kwenye Idara ya Utumishi anasema hivi: “Hii ni zawadi yenye ukarimu sana kutoka kwa Yehova. Ni jengo lililokusudiwa kutimiza mahitaji yetu. Tunashukuru sana kuwa na ofisi ya tawi maridadi na inayofaa kabisa.”
Tuna uhakika kwamba ofisi mpya ya Betheli itaboresha utendaji kazi na kuwa ushahidi mkubwa katika jamii, yote kwa utukufu wa Yehova.—2 Mambo ya Nyakati 7:1.
Familia ya Betheli ya Argentina ilihamia kwenye majengo ya ofisi mpya ya tawi huko Buenos Aires. Uhamaji huo uliofanywa kupatana na miongozo ya usalama ya COVID-19, ulianza Julai 2021. Baada ya kuhamia, Wanabetheli walimalizia kazi chache zilizohitaji kufanywa, kama vile kuunganisha vifaa ya mbao na kufanya usafi. Ofisi hiyo mpya itatoa ushahidi mkubwa katika jamii