Hamia kwenye habari

OKTOBA 14, 2019
ARGENTINA

Habari za Hivi Karibuni kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Betheli ya Argentina

Habari za Hivi Karibuni kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Betheli ya Argentina

Picha ya ofisi mpya ya tawi ya Argentina iliyochukuliwa wakati wa machweo

Mradi wa Ujenzi wa Tawi ya Ofisi ya Argentina umefikia nusu tangu ulipoanza zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Eneo hilo lina majengo matatu—jengo moja ni la ofisi na majengo mengine mawili ni ya makazi—yaliyo katika eneo lenye ukubwa wa mita 8,524 za mraba. Ujenzi unapaswa kukamilika Julai 2020.

Tunafurahi kuona maendeleo ya ujenzi wa Ofisi mpya ya Tawi ya Argentina. Tunasali kwamba Yehova aendelee kubariki mradi huu.—Kumbukumbu la Torati 28:8.

 

Aprili 2019: Mwonekano wa jengo la ofisi. Miimo inayoonekana katikati ya picha itapanda hadi kwenye orofa za juu ili kuhakikisha jengo hilo linasimama imara

Juni 2019: Mjenzi akiwa amesimama juu ya ngazi akiunganisha nondo kwa ajili ya mwimo wa jengo la Makazi A

Julai 2019: Wajenzi wakiunganisha nondo na vifaa vya umeme ndani ya sakafu ya orofa ya tatu ya jengo la ofisi

Julai 2019: Wajenzi wakimimina zege kwenye sakafu ya orofa ya pili ya jengo la Makazi A. Jengo hili litakuwa na orofa 5 na orofa ya tano na orofa ya mwisho itabaki wazi bila paa

Julai 2019: Mwonekano wa eneo la kuegesha magari. Eneo hilo limejengwa kuanzia chini ya ardhi ambapo kunaweza kuegeshwa magari 72 na linaendelea kwenye usawa wa ardhi ambapo linaweza kuegesha magari mengine 72

Agosti 2019: Picha inayoonyesha majengo ya Makazi A na Makazi B kwenye upande wa kushoto na jengo la ofisi linaonekana mwishoni, usawa wa greda