Hamia kwenye habari

Mchoro wa ofisi mpya ya tawi, ambayo itakuwa na jengo la ofisi na majengo mawili ya makazi. Familia ya Betheli inatazamiwa kuhamia huko mwezi wa sita wa mwaka wa 2020.

APRILI 29, 2019
ARGENTINA

Ujenzi Waanza Katika Ofisi Mpya ya Tawi Nchini Argentina

Ujenzi Waanza Katika Ofisi Mpya ya Tawi Nchini Argentina

Agosti 2018, ujenzi wa ofisi mpya ya tawi ulianza huko Buenos Aires, Argentina. Ujenzi huo utatia ndani jengo la ofisi lenye maeneo 136 ya kufanyia kazi na majengo mawili ya makazi yenye vyumba 98. Tofauti na ofisi ya tawi ya sasa ambayo imesambaa katika maeneo kadhaa tofauti-tofauti, majengo mapya yatakuwa katika eneo moja, na hivyo kuboresha utendaji wao. Picha zifuatazo zinaonyesha jinsi ujenzi ulivyoanza.

Eneo hilo lina ukubwa wa mita 8,524 za mraba na liko nje ya Buenos Aires, mji mkuu wa Argentina.

 

Agosti 2018: Kikosi cha kutoa michoro chenye ndugu na dada kumi kilifanya kazi kwa miezi 18 kutayarisha michoro ya ofisi hiyo.

Septemba 2018: Mashimo yalichimbwa ardhini ili kutayarisha msingi wa sehemu zitakazoongezwa. Kwa sababu ya mwinuko wa ardhi, mabomba 103 ya chuma yataingizwa kwenye kina cha mita 38 ili kuongeza uimara wa majengo.

Novemba 2018: Kreni yenye urefu wa mita 33 inatumiwa kwenye mradi huo.

Novemba 2018: Usalama ni jambo linalozingatiwa sana wakati wa kuunganisha kreni na linakaziwa katika muda wote wa mradi huo.

Januari 2019: Mashine zenye nguvu zinatumiwa kuchimba mifereji itakayotumiwa kwa ajili ya lifti.

Machi 2019: Msingi wa jengo moja unaimarishwa kabla ya zege kumwagwa.