MEI 2, 2017
ARGENTINA
Mvua Kubwa Zasababisha Uharibifu Nchini Argentina
BUENOS AIRES, Argentina—Kuanzia Machi 29, 2017, na kuendelea hadi Aprili 9, 2017, mvua kubwa ilisababisha mafuriko katika mikoa ya Argentina ya Buenos Aires, Chaco, Chubut, Catamarca, Jujuy, Misiones, La Pampa, Salta, San Juan, Santa Cruz, Santa Fe, Santiago del Estero, na Tucumán. Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova inaripoti kwamba hakuna Shahidi yeyote wa Yehova aliyeuawa au kuumia katika tukio hilo.
Maeneo yaliyoathiriwa sana na dhoruba hizo ni Chubut na Salta. Katika jiji la Comodoro Rivadavia, Chubut, kiwango cha mvua ambacho kwa kawaida kinanyesha mwaka mzima, kilinyesha kwa siku chache tu, na familia zaidi ya 60 za Mashahidi zililazimika kuondoka nyumbani kwao. Pia, majengo mawili ya ibada, au Majumba ya Ufalme, yaliharibiwa katika eneo la Chubut na lingine moja katika eneo la Salta. Ofisi ya tawi ya Argentina imeanzisha kamati ya kutoa msaada, katika mikoa yote miwili, kazi hiyo inatarajiwa kuisha baada ya majuma kadhaa.
Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:
David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000
Argentina: Omar A. Sánchez, +54-11-3220-5900