Hamia kwenye habari

DESEMBA 13, 2019
AUSTRALIA

Moto wa Msituni Waharibu Sehemu Kubwa ya Australia

Moto wa Msituni Waharibu Sehemu Kubwa ya Australia

Wenzi wa ndoa ambao ni Mashahidi wamepoteza nyumba yao baada ya moto wa msituni uliowaka mara kadhaa kwa nyakati tofauti kuunguza zaidi ya ekari milioni 2.5 huko New South Wales na Queensland nchini Australia. Hakuna ndugu yetu hata mmoja aliyekufa au kujeruhiwa kwa sababu ya moto huo. Pia Majumba ya Ufalme na Majumba ya Kusanyiko hayakuharibiwa na moto huo.

Wenye mamlaka wa eneo hilo wanashuku kwamba inawezekana sehemu ya moto huo ilisababishwa na watu fulani. Tangu mwezi Septemba, watu sita wamekufa na karibu nyumba 650 zimeharibiwa.

Karibu ndugu na dada 200 walilazimika kuhama makao yao, lakini tayari wamerudi katika nyumba zao kufikia sasa. Wenzi wa ndoa ambao nyumba yao iliharibiwa, wanatunzwa na Mashahidi wengine. Wazee wa makutaniko wanawapa kitia moyo kinachotegemea maandiko wote walioathiriwa na moto huo.—Matendo 20:28.