APRILI 6, 2017
AUSTRALIA
Australia Yakumbwa na Tufani Debbie
Jumanne, Machi 28, 2017, Tufani ya Kitropiki inayoitwa Debbie ilipiga pwani ya kaskazini mwa Queensland na visiwa vya karibu kwa upepo mkali unaovuma kwa kilomita 260 kwa saa. Tufani hiyo mbaya sana iliangusha miti, ikaharibu majengo, na kubeba mashua na kuzivunja kwenye fuo za miji iliyoko pwani. Pia, upepo uliovuma baada ya Tufani Debbie ulisababisha mafuriko katika miji na majiji ya kusini mwa Queensland na kaskazini mwa New South Wales, na kuwaacha maelfu ya wakazi bila umeme.
Ripoti za mapema zinaonyesha kwamba hakuna Shahidi wa Yehova aliyejeruhiwa au kuuawa. Hata hivyo, tufani hiyo iliharibu nyumba nyingi za Mashahidi na kubomoa moja kati ya hizo. Pia, Majumba mawili ya Ufalme (majengo ya ibada) yaliharibiwa.
Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Australia ilifanyiza halmashauri mbili za kutoa msaada ili kuratibu utendaji wa dharura, kuandaa jenereta, chakula, na maji kwa walioathiriwa. Pia wahudumu wa Mashahidi katika eneo hilo wanawatolea waabudu wenzao msaada wa kiroho na kihisia.
Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova linasimamia jitihada za kutoa msaada kutoka kwenye makao makuu ya ulimwenguni pote, kwa kutumia michango iliyotolewa kwa ajili ya kazi ya kuhubiri ulimwenguni pote.
Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:
David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000
Australasia: Rodney Spinks, +61-2-9829-5600