Hamia kwenye habari

DESEMBA 14, 2015
AZERBAIJAN

Azerbaijan Yapuuza Ombi la Umoja wa Mataifa la Kumhamisha Irina Zakharchenko

Azerbaijan Yapuuza Ombi la Umoja wa Mataifa la Kumhamisha Irina Zakharchenko

Serikali ya Azerbaijan imepuuza ombi la haraka la Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu la kuitaka imhamishe Irina Zakharchenko kutoka gerezani na kumpeleka kwenye hospitali au kumpa kifungo cha nyumbani. Desemba 10, 2015, juma moja baada ya serikali kupokea ombi hilo, hakimu wa kesi hiyo alikataa kumhamisha. Kwa sababu ya kufungwa gerezani kwa miezi kumi, Irina sasa ana utapiamlo, amekosa usingizi kwa muda mrefu, na amepatwa na athari kubwa ya kisaikolojia.

Pia, hakimu huyo alikataa ombi la kumhamisha Valida Jabrayilova, Shahidi ambaye pia anakabili mashtaka, na kumpa kifungo cha nyumbani.

Kesi hiyo itasikilizwa tena Desemba 17, 2015, kwenye Mahakama ya Wilaya ya Baku Pirallahi.