Hamia kwenye habari

DESEMBA 8, 2015
AZERBAIJAN

Azerbaijan Imehimizwa Kumhamisha Irina Zakharchenko Kutumikia Kifungo cha Nyumbani

Azerbaijan Imehimizwa Kumhamisha Irina Zakharchenko Kutumikia Kifungo cha Nyumbani

Desemba 3, 2015, Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu ilikubali ombi la haraka kwa niaba ya Irina Zakharchenko na kuiomba serikali ya Azerbaijan kumhamisha upesi kutoka gerezani hadi “kifungo cha nyumbani au kifungo kingine kinachofaa.” Ombi hilo lilitolewa kwa sababu ya afya yake inayozorota.

Irina Zakharchenko na Shahidi mwingine, Valida Jabrayilova, wamefungwa gerezani kwa miezi kumi kabla ya kesi yao kusikilizwa. Desemba 10, 2015, Mahakama ya Wilaya ya Baku Pirallahi itaanza kusikiliza kesi dhidi ya wanawake hao kwa shutuma za uhalifu wa kuwapa watu machapisho ya kidini na kushiriki imani yao “bila ruhusa.”