Hamia kwenye habari

JUNI 3, 2019
BOLIVIA

Maporomoko ya Ardhi Nchini Bolivia Yaharibu Eneo la La Paz

Maporomoko ya Ardhi Nchini Bolivia Yaharibu Eneo la La Paz

Aprili 30, 2019, maporomoko ya ardhi yaliharibu sehemu kubwa ya eneo la San Jorge Kantutani lililoko La Paz, Bolivia. Mamia ya watu waliachwa bila makao.

Ingawa hakuna ndugu aliyekufa au kujeruhiwa, ofisi ya tawi ya Bolivia inaripoti kwamba nyumba mbili za ndugu zetu ziliharibiwa kabisa wakati wa maporomoko hayo. Isitoshe, familia nyingine 11 za Mashahidi zinaishi katika eneo hilo lililoathiriwa lakini nyumba zao ziliharibiwa kidogo sana au hata hazikuathiriwa.

Chini ya mwongozo wa ofisi ya tawi, Halmashauri ya Kutoa Msaada, waangalizi wa mzunguko, na wazee wa eneo hilo wanaandaa msaada wa kiroho na wa kimwili. Akina ndugu katika maeneo yaliyoathiriwa wanatambua kwamba kunaweza kuwa na maporomoko zaidi ikiwa mvua itaendelea kunyesha.

Tunashukuru kwamba ndugu zetu hawakujeruhiwa na kwamba wanapokea msaada wanaohitaji.—Wagalatia 6:10.