Hamia kwenye habari

JANUARI 4, 2022
BRAZILI

Mvua Kubwa Yasababisha Mafuriko Kaskazini-Mashariki mwa Brazili

Mvua Kubwa Yasababisha Mafuriko Kaskazini-Mashariki mwa Brazili

Kuanzia Desemba 24 hadi 26, 2021, mvua kubwa ilinyesha katika Jimbo la Bahia nchini Brazili, na kuathiri zaidi ya watu 640,000. Mafuriko hayo yaliharibu mabwawa, na majiji kadhaa yakafurika na yakawa hayafikiki.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Hakuna ndugu aliyejeruhiwa

  • Wahubiri 273 wamelazimika kuhama makao yao

  • Nyumba 109 ziliharibiwa kidogo

  • Majumba 3 ya Ufalme yaliharibiwa kidogo

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Halmashauri ya Kutoa Msaada (DRC) ilianzishwa ili kuandaa maji, chakula, na mavazi

  • Kwa sasa wahubiri waliolazimika kuhama wanaishi na watu wa ukoo au na wahubiri wengine

  • Jitihada zote za kutoa msaada zinatolewa kupatana na miongozo ya kujilinda dhidi ya COVID-19

Ndugu Marcelo Ambrósio, anayetumikia kwenye DRC, anasema hivi: “Upendo tunaoona miongoni mwa ndugu zetu, umetutia moyo sana na unatuchochea kumtumikia Yehova kikamili zaidi.”

Tunajua kwamba Yehova atakuwa“kimbilio salama” kwa ajili ya ndugu zetu walioathiriwa na dhoruba.​—Zaburi 9:9.