Hamia kwenye habari

Mvua kubwa na maporomoko ya ardhi yasababisha uharibifu mkubwa katika jiji la milimani la Petrópolis

FEBRUARI 23, 2022
BRAZILI

Mvua Kubwa na Maporomoko ya Ardhi Yasababisha Uharibifu Mkubwa Katika Jiji Lililo Milimani Nchini Brazili

Mvua Kubwa na Maporomoko ya Ardhi Yasababisha Uharibifu Mkubwa Katika Jiji Lililo Milimani Nchini Brazili

Februari 15, 2022, mvua kubwa ilisababisha maporomoko hatari ya ardhi katika jiji la milimani la Petrópolis lililo kwenye jimbo la Rio de Janeiro, nchini Brazili. Nyumba na biashara ziliharibiwa. Mvua kubwa kiasi cha sentimita 26, ilinyesha ndani ya saa 24 tu.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Ndugu mmoja alijeruhiwa vibaya na akapelekwa hospitali ya karibu. Kwa kusikitisha mwana wake mwenye umri wa miaka 2 alikufa baada ya kusombwa na maporomoko ya ardhi

  • Ndugu mwingine 1 alikufa

  • Wahubiri 86 wamelazimika kuhama makao yao

  • Nyumba 2 ziliharibiwa kabisa

  • Nyumba 15 zilipata uharibifu mkubwa

  • Majumba 2 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Halmashauri ya Kutoa Msaada ilianzishwa ili kupanga kazi ya kutoa msaada

  • Mwangalizi wa mzunguko na wazee wa makutaniko wanawapatia akina ndugu walioathiriwa chakula, maji, nguo, na pia kuwategemeza kiroho

  • Kwa sasa ndugu na dada waliolazimika kuhama makao yao wanaishi na watu wao wa ukoo au familia nyingine za Mashahidi

  • Jitihada zote za kutoa msaada zinafanywa kupatana na miongozo ya kujilinda dhidi ya ugonjwa wa COVID-19

Tunapoendelea kusali kwa ajili ya ndugu na dada zetu walioathiriwa na msiba huo, tunajua kwamba Yehova ‘ataifariji mioyo yao na kuwaimarisha,’ hasa waliofiwa na wapendwa wao.​—2 Wathesalonike 2:16, 17.