Hamia kwenye habari

JULAI 18, 2019
BRAZILI

São Paulo, Brazili—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”!

São Paulo, Brazili—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”!
  • Tarehe: Julai 12-14, 2019

  • Mahali: Eneo la Maonyesho ya Kimataifa jijini São Paulo, Brazili

  • Lugha za Programu: Lugha ya Ishara ya Brazili, Kiingereza, Kifaransa, Kiitaliano, Kireno na Kihispania

  • Idadi ya Wahudhuriaji: 36,624

  • Idadi ya Waliobatizwa: 291

  • Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 7,000

  • Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Angola, Argentina, Ubelgiji, Czech-Slovak, Ufaransa, Italia, Msumbiji, Ureno, Skandinavia, Suriname, Trinidad na Tobago, Marekani, Venezuela

  • Mambo Yaliyoonwa: Bi. Maria Luiza Gonçalves, msemaji wa eneo la bustani ya wanyama iliyoko jijini São Paulo, ambaye aliwakaribisha wajumbe, alisema hivi: “Watu wengi wametembelea bustani hii ya wanyama. Tunapokea watalii kila mwaka, lakini sijawahi kuona kikundi kama chenu ambacho kina watu wengi, wenye uchangamfu na wanaofuata utaratibu. Ninyi mna upendo mwingi sana! Mnaonyesha upendo kwa kukumbatiana, kuonyeshana urafiki, na kuimba.”

 

Ndugu na dada wenyeji wakiwakaribisha wajumbe waliowasili kwenye uwanja wa ndege wa Guarulhos jijini São Paulo

Ndugu wanne kutoka katika ofisi ya tawi ya Brazili wakizungumza na waandishi wa habari ili kuelezea mapema manufaa ya kusanyiko la kimataifa

Wajumbe wakihubiri pamoja na wenyeji wao katika jiji la São Paulo

Wajumbe wakiwa nje ya uwanja wa kusanyiko siku ya kwanza ya kusanyiko

Ndugu na dada wakiandika mambo makuu wakati wa programu ya kusanyiko

Ndugu Samuel Herd, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akitoa hotuba ya mwisho ya programu ya Ijumaa

Akina ndugu wakibatiza siku ya Jumamosi mchana

Akina dada wakiwatafsiria programu kwa mikono wahudhuriaji ambao ni vipofu na viziwi

Wajumbe wakipiga picha nje ya uwanja wa kusanyiko

Watumishi wa wakati wote wa pekee waliotembelea wakiwapungia mkono wasikilizaji mwishoni mwa programu ya Jumapili