Matukio Muhimu Kihistoria Nchini Bulgaria
MEI 19, 2004—ECHR iliunga mkono Mashahidi katika kesi ya Lotter and Lotter v. Bulgaria; serikali iliidhinisha haki ya kisheria ya Mashahidi kushiriki katika utendaji wa kidini na kuwajulisha wengine imani yao bila kuvurugwa
APRILI 16, 2003—Serikali ilitambua Ukumbusho wa kifo cha Kristo kuwa sikukuu rasmi ya Mashahidi wa Yehova na kuwaruhusu Mashahidi wachukue likizo kutoka kazini
MACHI 6, 2003—Mashahidi wa Yehova walisajiliwa chini ya Sheria mpya ya Madhehebu ya Dini
MEI 3, 2001—ECHR ilikubali suluhisho lililounga mkono mmoja wa Mashahidi wa Yehova katika kesi (Stefanov v. Bulgaria); serikali iliwapa masamaha wale wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri ikiwa wako tayari kufanya utumishi wa badala wa kiraia
OKTOBA 7, 1998—Mashahidi wa Yehova walisajiliwa rasmi nchini Bulgaria
MACHI 9, 1998—Kwa sababu ya makubaliano ambayo yalikubaliwa na Tume ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (sasa ni Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu [ECHR]), serikali ya Bulgaria ilikubali kuwaandikisha kisheria Mashahidi wa Yehova kuwa dini inayotambulika
1994—Bulgaria yafutilia mbali kusajiliwa kwa Mashahidi wa Yehova baada ya kupitisha sheria kali kuhusu dini
MEI 7, 1992—Bulgaria inakuwa nchi ya 26 kujiunga na Baraza la Ulaya
JULAI 17, 1991—Serikali yasajili rasmi Shirika la Christian Association of Jehovah’s Witnesses
1944-1990—Utendaji wa Mashahidi wa Yehova wapigwa marufuku chini ya utawala wa Kikomunisti
MEI 6, 1938—Mashahidi wa Yehova watambuliwa kisheria
1888—Rekodi za kale zaidi za utendaji wa Mashahidi wa Yehova zinaanzia mwaka huu nchini Bulgaria