Hamia kwenye habari

SEPTEMBA 12, 2023
CHILE

Chile Kusini Yakumbwa na Mafuriko Makubwa

Chile Kusini Yakumbwa na Mafuriko Makubwa

Kuanzia Agosti 19 hadi Agosti 23, 2023, upande wa kusini wa Chile ulikumbwa na dhoruba zenye nguvu zilizosababisha mafuriko makubwa. Kwa kusikitisha, mafuriko hayo ya karibuni yamewaathiri wengi kati ya ndugu na dada zetu ambao tayari walikuwa wameathiriwa na mafuriko yaliyotokea katika eneo hilohilo mnamo Juni 2023. Ripoti zinaonyesha kwamba hicho ndicho kiasi kikubwa zaidi cha mvua kunyesha katika eneo hilo katika miaka 10 iliyopita. Maeneo mengi yamekumbwa na ongezeko la mvua na pia mafuriko kwa sababu ya kuongezeka kwa kiwango cha joto katika maji ya Bahari ya Pasifiki, pamoja na hali ya hewa inayoitwa El Niño. Nyumba 25,000 hivi zimeharibiwa, na watu watatu wamekufa.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Mafuriko yaliharibu nyumba ya ndugu iliyotumiwa kufanyia mikutano

    Hakuna ndugu au dada ambaye amekufa au kujeruhiwa

  • Wahubiri 225 walihitaji kuhama makao yao

  • Nyumba 13 zilipata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 38 zilipata uharibifu mdogo

  • Majumba 3 ya Ufalme na nyumba moja ya ndugu inayotumiwa kufanyia mkutano zilipata uharibifu mdogo

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Waangalizi wa mzunguko na wazee wa eneo hilo wanatoa msaada wa kiroho na wa kimwili kwa wote katika maeneo yaliyoathiriwa

  • Halmashauri 2 za Kutoa Msaada zimewekwa rasmi ili kusimamia kazi ya kutoa msaada

Tunasali kwa ajili ya ndugu na dada zetu walioathiriwa na mafuriko nchini Chile na tunatazamia kwa hamu wakati ambapo Ufalme wa Mungu utatawala na hakutakuwa tena na majanga kama hayo.​—Isaya 32:18.