Hamia kwenye habari

Maji ya mvua yalivyofurika Doñihue (kushoto) na Linares (kulia), nchini Chile

JULAI 6, 2023
CHILE

Mafuriko Makubwa Yaathiri Makumi ya Maelfu ya Watu Nchini Chile

Mafuriko Makubwa Yaathiri Makumi ya Maelfu ya Watu Nchini Chile

Kuanzia Juni 22 hadi 25, 2023, mvua kubwa zilinyesha kusini mwa Chile na katika maeneo ya kati kufikia kipimo cha sentimita 58. Watu 20,000 hivi wameathiriwa na mafuriko hayo. Zaidi ya nyumba 5,000 zilizo katika maeneo hayo zimepata uharibifu mdogo na nyingine uharibifu mkubwa. Maelfu ya watu wanaendelea kuhama makazi yao. Kufikia sasa, ripoti zinaonyesha watu wawili wamekufa na watu wengine wawili wamepotea.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Hakuna ndugu aliyejeruhiwa au kuuawa

  • Wahubiri 212 wamelazimika kuhama makao yao

  • Nyumba 13 zilipata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 38 zilipata uharibifu mdogo

  • Hakuna Jumba la Ufalme au jengo lolote la kitheokrasi lililopata uharibifu

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Mamia ya wajitoleaji wanasaidia kufanya usafi na kurekebisha nyumba zilizopata uharibifu

  • Waangalizi wa mzunguko na wazee wa makutaniko wanashirikiana ili kuwaandalia wale walioathiriwa msaada wa kiroho na wa kimwili

  • Halmashauri 2 za Kutoa Msaada ziliteuliwa ili kusimamia jitihada za kutoa msaada

Tunasali kwamba Yehova aendelee kuwafariji na kuwaimarisha ndugu na dada zetu nchini Chile wanapoendelea kukabiliana na athari za janga hili.​—2 Wathesalonike 2:16, 17.