Hamia kwenye habari

Magofu ya nyumba ya dada katika jiji la Tomé, Eneo la Biobío

FEBRUARI 17, 2023
CHILE

Mioto Yasababisha Uharibifu Mkubwa Katikati mwa Chile

Mioto Yasababisha Uharibifu Mkubwa Katikati mwa Chile

Kwa mara ya pili ndani ya miaka kumi, mioto mibaya sana imesababisha uharibifu mkubwa nchini Chile. Wenye mamlaka wameripoti zaidi ya mioto 300 nchini kote kuanzia mapema Februari 2023. Kufikia sasa bado mioto mingi inaendelea. Imeharibu zaidi ya ekari 1,062,553 za ardhi katika maeneo ya katikati ya Araucanía, Biobío, na Ñuble. Inaripotiwa kwamba miundombinu muhimu nchini humo imeharibiwa kutia ndani barabara kuu na hospitali. Watu 6,000 hivi wameathiriwa na mioto hiyo, na zaidi ya nyumba 1,500 imeharibiwa. Kufikia sasa imeripotiwa kwamba watu 25 wamekufa.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Mioto ikiwaka katika mji wa Ñipas, Eneo la Ñuble, nchini Chile

    Hakuna ndugu au dada yetu ambaye amekufa

  • Wahubiri 222 walilazimika kuhama; 76 bado hawajapata makao

  • Nyumba 18 ziliharibiwa

  • Hakuna Jumba la Ufalme ambalo liliharibiwa

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Wazee wa eneo hilo pamoja na waangalizi wa mzunguko wanaandaa utegemezo wa kiroho wenye upendo kwa wale walioathiriwa na msiba huo

  • Halmashauri ya Kutoa Msaada imewekwa rasmi ili kuratibu jitihada za kutoa msaada

Katika hali hizo ngumu, ndugu na dada zetu wanaweza kuwa na uhakika kwamba Yehova, “ambaye hutufariji katika majaribu yetu yote,” yuko karibu nao.​—2 Wakorintho 1:4.