Hamia kwenye habari

ERITREA

Matukio Muhimu Kihistoria Nchini Eritrea

Matukio Muhimu Kihistoria Nchini Eritrea
  1. APRILI 2014—Wenye mamlaka wakamata zaidi ya Mashahidi 120 (wanaume, wanawake, na watoto) kwa sababu ya kuhudhuria mikutano ya kidini; wengi wao waliachiliwa huru baadaye

  2. JULAI 8, 2008—Wenye mamlaka wavamia nyumba na maeneo ya kazi ya Mashahidi na kukamata Mashahidi 24

  3. MEI 2002—Serikali yapiga marufuku vikundi vyote vya kidini isipokuwa vikundi vinne vinavyotambuliwa na serikali

  4. OKTOBA 25, 1994—Mashahidi wa Yehova wapoteza uraia wao na haki zilizowalinda kama raia kwa sababu ya amri iliyotolewa na rais wa Eritrea

  5. SEPTEMBA 17, 1994—Wenye mamlaka waliwakamata Paulos Eyassu, Isaac Mogos, na Negede Teklemariam bila kuwafungulia mashtaka yoyote

  6. 1994—Wenye mamlaka waanza kuwakamata na kuwafunga Mashahidi wa Yehova

  7. APRILI 27, 1993—Eritrea yapata uhuru kutoka Ethiopia

  8. 1954—Kikundi kidogo cha Mashahidi wa Yehova chaanza kufanya ibada