Hamia kwenye habari

MACHI 13, 2019
ETHIOPIA

Dada Amekufa Katika Ndege Iliyoanguka ya Ethiopian Airlines

Dada Amekufa Katika Ndege Iliyoanguka ya Ethiopian Airlines

Jumapili, Machi 10, ndege ya Ethiopian Airlines Namba 302 ilianguka muda mfupi baada ya kutoka Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia. Watu wote 157 waliokuwa ndani ya ndege hiyo walikufa.

Inasikitisha kwamba dada yetu mmoja, Rosemary Mumbi, alikuwa miongoni mwa watu waliokufa katika aksidenti hiyo. Dada Mumbi alikuwa na umri wa miaka 66 na alikuwa mhudumu wa wakati wote katika Kutaniko la Roma Manzoni Inglese jijini Rome, Italia.

Tunahuzunika sana kupata habari za kifo hicho. Tunatazamia kwa hamu ufufuo, wakati ambapo tutawakaribisha watumishi waaminifu wa Yehova, kutia ndani Dada Mumbi.—Ufunuo 20:13.