JANUARI 7, 2021
FIJI
Kimbunga Yasa Chapiga Fiji
Mahali
Fiji
Janga
Alhamisi, Desemba 17, 2020, Kimbunga Yasa cha Kitropiki kilisababisha maporomoko ya ardhi katika Vanua Levu, kisiwa cha pili kwa ukubwa nchini Fiji
Yasa ni kimbunga cha pili chenye nguvu zaidi kuwahi kuipiga Fiji. Inaripotiwa kwamba upepo mkali ulivuma kufikia mwendo wa kilomita 260 kwa saa
Kuna makutaniko 30 na vikundi vilivyo katika maeneo ya mbali kwenye maeneo hayo yaliyoathiriwa
Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata
Hakuna ndugu au dada waliojeruhiwa
Taarifa za awali zinaonyesha kwamba familia 20 zililazimika kuhama makazi yao
Kimbunga hicho kilileta uharibifu mkubwa wa mazao na hivyo kuharibu chanzo kikuu cha chakula kwa wahubiri 430 katika eneo hilo
Uharibifu wa mali
Nyumba 10 zimepata uharibifu mkubwa
Nyumba 25 zimeharibiwa
Jumba la Ufalme 1 limeharibiwa kidogo
Jitihada za kutoa msaada
Ofisi ya tawi ya Fiji imeweka rasmi Halmashauri tatu za Kutoa Msaada (DRC). Halmashauri hizo zimesaidia kutoa msaada wa kibinadamu kwa wahubiri walioathiriwa kwa kuwapa maji safi ya kunywa, mavazi, chakula na turubai. Kwa kuongezea halmashauri hizo zimewasaidia kupata makazi ya muda wale waliolazimika kuhama makazi yao
Wawakilishi kutoka ofisi ya tawi ya Fiji pamoja na waangalizi wa mzunguko wanafanya ziara za uchungaji kwa walioathiriwa na kimbunga hicho
Wote wanaohusika katika kazi ya kutoa msaada na kufanya ziara za uchungaji wanafuata miongozo yote ya kujilinda dhidi ya ugonjwa wa COVID-19
Ingawa ndugu na dada zetu wameathiriwa na kimbunga hicho, wanajionea ukweli wa maneno ya Zaburi 46:1: “Mungu ni kimbilio letu.”