Hamia kwenye habari

JANUARI 15, 2013
FIJI

Tufani ya Kitropiki ya Evan Yapiga Visiwa vya Pasifiki ya Kusini

Tufani ya Kitropiki ya Evan Yapiga Visiwa vya Pasifiki ya Kusini

Suva, FIJI—Katikati ya mwezi wa Desemba 2012, tufani mbaya sana ya kitropiki ilipiga kisiwa cha Fiji na Samoa. Tufani inayoitwa Evan, inayotajwa kuwa mojawapo ya tufani kubwa zaidi iliyowahi kupiga Fiji katika kipindi cha miaka 70 iliyopita, iliharibu eneo kubwa, ilibomoa majengo na barabara na kusababisha maelfu ya watu kuhama makwao. Mtu mmoja alilinganisha uharibifu uliosababishwa na tufani hiyo na ile tsunami iliyotokea kwa ghafula katika mwaka wa 2009.

Hakuna Shahidi yeyote wa Yehova aliyeripotiwa kufa au kuumizwa na tufani hiyo. Hata hivyo, tufani hiyo imeharibu nyumba nyingi za Mashahidi. Huko Fiji, makadirio ya mwanzoni yalionyesha kwamba zaidi ya nyumba 80 za Mashahidi ziliharibiwa au kubomolewa kabisa. Katika kisiwa cha Samoa kinachoitwa Upolu, Mashahidi 47 walihama makwao kwa sababu ya kimbunga hicho.

Waathiriwa wa huko Samoa walipewa makao ya muda katika nyumba za ibada za eneo hilo zinazotumiwa na Mashahidi wa Yehova, na wengine waliishi na familia za Mashahidi wenzao. Misaada zaidi huko Samoa imetolewa na ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Australia. Kufikia Desemba 18, chakula na misaada mingine ilikuwa imegawanywa katika makutaniko manne na ofisi moja ya utafsiri ya Mashahidi wa Yehova ilitumiwa kuhifadhi maji safi. Kikundi cha Mashahidi pia kilisaidia kurekebisha nyumba zilizoharibiwa na pia kusafisha na kuondoa uchafu katika nyumba hizo zilizojaa maji na matope. Huko Fiji, mahitaji ya dharura ya waathiriwa wa dhoruba yalishughulikiwa na halmashauri za kutoa misaada za Mashahidi waliojitolea. Halmashauri hizo zinapanga pia jinsi ya kuwasaidia hata zaidi Mashahidi ambao mazao yao yaliharibiwa na dhoruba hiyo.

Tevita Sadole, msemaji wa Mashahidi wa Yehova nchini Fiji, alisema hivi: “Ingawa tuna kazi nyingi sana za kufanya baada ya msiba huu kutokea, bado tunakabiliana na hali hii vizuri. Tunatazamia hata zaidi kuwasaidia washiriki wenzetu na jirani zetu katika siku zijazo.”

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000

Australia: Donald MacLean, simu +61 2 9829 5600

Fiji: Tevita Sadole, simu +679 330 4766