Hamia kwenye habari

Nyumba mbili za Mashahidi zilizoharibiwa na dhoruba.

JANUARI 22, 2019
FILIPINO

Dhoruba ya Kitropiki Yatokeza Maporomoko ya Ardhi na Mafuriko Filipino Mashariki

Dhoruba ya Kitropiki Yatokeza Maporomoko ya Ardhi na Mafuriko Filipino Mashariki

Desemba 29, 2018, Dhoruba ya Kitropiki Usman ilipiga kisiwa cha Samar, kisiwa cha tatu kwa ukubwa nchini Filipino. Kulikuwa na mvua kubwa iliyosababisha maporomoko ya ardhi na mafuriko ya ghafla. Watu 25 hivi wamekufa, na 42 wakajeruhiwa. Na nyumba 22,835 zimeharibiwa na dhoruba hiyo.

Ofisi ya tawi ya Filipino imeripoti kwamba hakuna ndugu au dada aliyekufa kutokana na dhoruba hiyo. Hata hivyo, nyumba tatu za akina ndugu zimeharibiwa kabisa, na nyumba nne zimeharibiwa kwa kadiri fulani. Kwa kuongezea, Jumba moja la Ufalme limeharibiwa. Chini ya mwongozo wa ofisi ya tawi, Halmashauri ya Kutoa Misaada iliandaa mahitaji na makazi ya muda kwa familia zilizoathiriwa na dhoruba hiyo.

Tuna uhakika kwamba ndugu na dada zetu walioathiriwa na dhoruba hiyo wataendelea kumtegemea Yehova, wakijua kwamba atawaimarisha na kuwapa nguvu.—1 Petro 5:10.