Hamia kwenye habari

Kimbunga Noru chasababisha mafuriko makubwa nchini Filipino

OKTOBA 6, 2022
FILIPINO

Kimbunga Noru Chapiga Filipino

Kimbunga Noru Chapiga Filipino

Septemba 25, 2022, Kimbunga Noru, kinachojulikana kiasili kama Karding, kilisababisha uharibifu mkubwa katika kisiwa cha Polillo kilicho katika Jimbo la Quezon, nchini Filipino. Baada ya muda mfupi kimbunga hicho kilifika katika Jimbo la Aurora. Kimbunga hicho kiliambatana na upepo mkali uliosonga kwa kasi ya kilometa 195 kwa saa, pia, kulikuwa na upepo uliovuma kwa kasi ya kilometa 240 kwa saa. Kimbunga Noru killisababisha uharibifu mkubwa wa nyumba, barabara na madaraja na kusababisha mafuriko makubwa.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Hakuna ndugu au dada ambaye amekufa

  • Familia 180 zimelazimika kuhama makazi yao

  • Nyumba 209 zimepata uharibifu mdogo

  • Nyumba 20 zimepata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 22 zimeharibiwa kabisa

  • Majumba 7 ya Ufalme yamepata uharibifu mdogo

  • Jumba 1 la Ufalme limepata uharibifu mkubwa

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Halmashauri 2 za Kutoa Msaada zimeanzishwa

  • Wazee wa makutaniko wanafanya ziara za uchungaji kwa ndugu na dada walioathiriwa na kuandaa msaada unaohitajika

  • Jitihada zote za kutoa msaada, zinafanywa kupatana na miongozo ya kujilinda dhidi ya ugonjwa wa COVID-19

Tunaendelea kusali kwa ajili ya akina ndugu waliokumbwa na kimbunga ili Yehova awe kimbilio lao—Zaburi 57:1.