OKTOBA 31, 2024
FILIPINO
Kimbunga Trami Chaipiga Filipino
Oktoba 21, 2024, Kimbunga Trami a kilisababisha uharibifu mkubwa nchini Filipino. Kimbunga hicho kilikuwa na nguvu zaidi katika maeneo ya kaskazini mwa nchi na kilisababisha upepo mkali uliovuma kwa kilomita 160 kwa saa. Upepo mkali na mvua kubwa zilizotokana na kimbunga hicho zilisababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyoharibu nyumba, barabara, na kufanya watu wakose umeme na maji. Kati ya watu milioni sita wanaoishi katika eneo lililoathiriwa, milioni moja walilazimika kuhama makazi yao. Watu 126 hivi walikufa.
Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata
Kwa kusikitisha, dada mmoja alikufa
Wahubiri 747 walilazimika kuhama makazi yao
Nyumba 7 ziliharibiwa kabisa
Nyumba 24 zilipata uharibifu mkubwa
Nyumba 128 zilipata uharibifu mdogo
Majumba 8 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo
Jitihada za Kutoa Msaada
Waangalizi wa mzunguko na wazee wa eneo hilo, wanaendelea kushughulikia mahitaji ya kiroho na ya kimwili ya walioathiriwa na kimbunga hicho
Halmashauri 5 za Kutoa Msaada zinasimamia jitihada za kutoa msaada
Tunasikitishwa na vifo na uharibifu uliosababishwa na kimbunga hicho. Hata hivyo, ahadi ya Biblia kwamba mambo hayo hayatakuwepo tena, inaendelea kutufariji na kutupatia tumaini.—Isaya 25:8.
a Nchini Filipino kimbunga hicho kinaitwa Kristine.