AGOSTI 5, 2019
FILIPINO
Matetemeko ya Ardhi Yatikisa Ufilipino
Mnamo Julai 27, 2019, matetemeko mawili ya ardhi yalitokea katika kisiwa kidogo cha Itbayat nchini Ufilipino, kilomita 690 hivi upande wa kaskazini wa Manila. Matetemeko hayo yalikuwa ya kiwango cha 5.4 na 6.4. Watu 9 walikufa, 64 wakajeruhiwa, na nyumba 266 zikaharibiwa. Ripoti zinaonyesha kwamba watu 2,968 waliathiriwa na matetemeko hayo.
Hakuna ndugu zetu waliokufa kutokana na matetemeko hayo. Hata hivyo, dada mmoja alipata majeraha madogo. Vilevile, kulikuwa na uharibifu mkubwa wa nyumba mbili za ndugu zetu.
Ofisi ya tawi iliunda Halmashauri ya Kutoa Msaada, ambayo inasaidia katika ununuzi na usambazaji wa bidhaa za msingi kama vile chakula na maji. Wawakilishi kutoka ofisi ya tawi watawatembelea ndugu na dada walioathiriwa ili kuwafariji kiroho na kutoa msaada unaohitajika.
Tunasali kwa ajili ya ndugu na dada zetu walioathiriwa na matetemeko ya ardhi yaliyotokea hivi karibuni. Tunajua kwamba Yehova, “Mungu wa faraja yote,” ataendelea kuwaandalia ndugu zetu mahitaji yao.—2 Wakorintho 1:3.