Hamia kwenye habari

Nyumba za ndugu zetu zilizoharibiwa na moto katika mji wa Taguig, Metro Manila

MEI 21, 2019
FILIPINO

Moto Waharibu Nyumba Nchini Filipino

Moto Waharibu Nyumba Nchini Filipino

Machi 2019, moto uliwaka na kuharibu nyumba 128 katika Jiji la Calbayog kwenye Kisiwa cha Samar. Mwezi uliotangulia, kulikuwa na moto katika Jiji la Taguig kwenye Kisiwa cha Luzon. Jumla ya nyumba saba za Mashahidi wa Yehova ziliteketezwa na mioto hiyo. Ndugu na dada zetu waliopoteza makao wanaishi na Mashahidi wengine ambao hawakuathiriwa na mioto hiyo.

Ofisi ya tawi ilichukua hatua haraka kwa kuandaa chakula, maji, na mavazi. Wazee wa eneo hilo walifanya ziara za uchungaji kwa kuwatembelea ndugu waliothiriwa na janga hilo na kuwasaidia na mahitaji yao ya kimwili. Kwa msaada wa halmashauri mbili za kutoa msaada pamoja na idara ya Usanifu-Majengo na Ujenzi wanajiandaa kujenga upya nyumba za waabudu wenzetu.

Tunatumaini kwamba Yehova ataendelea kuwa kimbilio kwa ajili ya ndugu zetu ambao waliathiriwa na moto.—Zaburi 62:8.