AGOSTI 5, 2022
FILIPINO
Tetemeko Kubwa Lakumba Filipino Kaskazini
Julai 27, 2022, tetemeko lenye kipimo cha 7.0 lilitokea katika kisiwa cha Luzon, nchini Filipino. Mkoa wa Abra ndio ulioathiriwa zaidi. Mji wa Manila ulio kilomita 400 hivi kutoka Luzon pia ulipatwa na matetemeko madogo. Tetemeko hilo la ardhi lilifuatiwa na matetemeko mengine madogo-madogo zaidi ya 2,000.
Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata
Hakuna ndugu au dada aliyejeruhiwa
Wahubiri 4 walipata majeraha madogo
Familia 42 zililazimika kuhama makazi yao
Nyumba 63 zilipata uharibifu mdogo
Nyumba 1 ilipata uharibifu mkubwa
Majumba 13 ya Ufalme yamepata uharibifu
Jitihada za Kutoa Msaada
Halmashauri 1 ya Kutoa Msaada iliteuliwa ili kusimamia kazi ya kutoa msaada
Wazee wa eneo hilo wanawafanyia ziara za uchungaji wale walioathiriwa
Jitihada zote za kutoa msaada zinafanywa kupatana na miongozo ya kujilinda na COVID-19
Bila kukawia, ofisi ya tawi ilituma bidhaa mbalimbali za msaada kwa ndugu na dada kwenye maeneo yaliyoathiriwa na kuwaandalia makazi ya muda. Katika maeneo hayo, wahubiri walisaidiana wenyewe licha ya kwamba wote walikuwa wameathiriwa na tetemeko hilo.
Tuna imani kabisa kwamba Yehova atawaokoa ndugu na dada zetu katika ‘wakati huu wa taabu.’—Zaburi 50:15.