Hamia kwenye habari

NOVEMBA 12, 2018
FILIPINO

Kimbunga Yutu Kinaendelea, Kimeipiga Filipino

Kimbunga Yutu Kinaendelea, Kimeipiga Filipino

Jumanne Oktoba 30, Kimbunga Yutu kiliipiga Luzon, kisiwa kikubwa zaidi nchini Filipino. Oktoba 24 kimbunga hichohicho kilikuwa kimepita kwenye Visiwa vya Mariana Kaskazini. Mvua kubwa iliyotokezwa na kimbunga hicho ilisababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyowaua watu wengi. Maelfu ya watu walilazimika kuhamishwa, na 11 walikufa.

Ofisi ya tawi ya Filipino inaripoti kwamba hakuna ndugu au dada aliyekufa au kujeruhiwa katika dhoruba hiyo. Hata hivyo, nyumba 73 za ndugu zetu ziliharibiwa kutia ndani Majumba 6 ya Ufalme. Ofisi ya tawi ya Filipino inaratibu kazi ya kutoa msaada.

Tunaendelea kusali kwa ajili ya ndugu na dada zetu nchini Filipino, ambao wameathiriwa na vimbunga 18 mwaka huu. Kwa pamoja, tuna uhakika kwamba Yehova anajua jinsi ya kututegemeza.—Zaburi 55:22.