Hamia kwenye habari

GEORGIA

Maelezo Mafupi Kuhusu Georgia

Maelezo Mafupi Kuhusu Georgia

Mashahidi wa Yehova wameanza utendaji wao nchini Georgia mwaka 1953. Wamesajiliwa kisheria na kwa ujumla wanafurahia uhuru wa ibada. Pamoja na hayo, bado matatizo kuna yanayotokana na ubaguzi wa kidini.

Kuanzia mwaka 1999 hadi 2003, watu wenye msimamo mkali wa kidini waliwashambulia vikali Mashahidi wa Yehova. Washambuliaji hao walichochewa kufanya hivyo kwa kuwa vyombo vinavyotekeleza sheria vimekataa kuwaadhibu kwa kuvunja kisheria. Wakati huo, mwanaharakati mmoja ambaye pia ni mbunge alifanikiwa kuishawishi serikali isimamishe usajili wa shirika la Mashahidi kwa muda, jambo lililosababisha Mashahidi waendelee kufanyiwa vurugu. Mashahidi walifungua kesi sita katika Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu (ECHR) ili kushughulikia matatizo hayo. Katika mwaka 2007 na 2014, Mahakama ya ECHR ilitoa uamuzi ulioshutumu serikali kwa kushindwa kushughulikia mara moja na bila ubaguzi uhalifu unaochochewa na chuki ya kidini. Katika mwaka 2015, ECHR ilitoa uamuzi na kusema kwamba serikali haikutenda haki iliposimamisha usajili wa mashirika ya Mashahidi nchini Georgia mwaka 2001.

Kuanzia mwaka 2004, mashambulizi dhidi ya Mashahidi wa Yehova yamepungua kwa kiasi kikubwa. Hivyo, wameweza kupanua utendaji wao na kujenga Majumba ya Ufalme. Hata hivyo, wakati mwingine bado wananyanyaswa na kufanyiwa uhalifu unaochochewa na chuki ya kidini. Tatizo hilo haliishi kwa kuwa mara nyingi mamlaka za serikali hazichukui hatua dhidi ya matendo hayo ya uhalifu. Mashahidi wanatarajia kwamba serikali ya Georgia itatii kabisa maamuzi ya ECHR kwa kupeleleza matendo hayo ya jeuri mara moja na kuwashtaki wanaohusika.