Hamia kwenye habari

Nyumba za ndugu na dada zetu zilizopata uharibifu katika kijiji cha Dededo, Guam

JUNI 19, 2023
GUAM

Kimbunga Mawar Chapiga Guam na Rota

Kimbunga Mawar Chapiga Guam na Rota

Mei 24, 2023, Kimbunga Mawar kilipiga visiwa vya Guam na Rota. Kimbunga hicho kilikuwa na nguvu kuliko kimbunga kingine chochote ambacho kimepita kwenye eneo hilo katika miaka 20 iliyopita. Mvua kubwa zilinyesha na kipimo chake kilikuwa zaidi ya sentimeta 70 (inchi 28) na upepo ulivuma kwa kasi ya zaidi ya kilomita 160 kwa saa. Upepo huo na mvua hizo kubwa zilisababisha uharibifu mwingi kutia ndani kukatika kwa umeme na maji katika sehemu nyingi za Guam na Rota.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Hakuna ndugu au dada yetu aliyejeruhiwa au kufa

  • Nyumba 3 ziliharibiwa kabisa

  • Nyumba 12 zilipata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 8 zilipata uharibifu mdogo

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Waangalizi wa mzunguko wanashirikiana na wazee wa makutaniko ya maeneo hayo ili kuwapa wale walioathiriwa msaada wa kiroho na wa kimwili

  • Halmashauri 2 za Kutoa Msaada zilianzishwa ili kusimamia kazi ya kutoa msaada

Tunatazamia kwa hamu wakati ambapo hakuna mtu atakayeishi akiwa na hofu ya majanga ya asili bali watu wote “watafurahia kwelikweli wingi wa amani.”​—Zaburi 37:11.