Hamia kwenye habari

JUNI 5, 2018
GUATEMALA

Volkano Yalipuka Nchini Guatemala

Volkano Yalipuka Nchini Guatemala

Jumapili, Juni 3, 2018, Volcan de Fuego ya Guatemala, au “volkano ya moto,” ililipuka, ikamwaga lava na kurusha moshi kilomita 9 hewani. Kuna makutaniko kumi hivi katika eneo lililoathiriwa. Tunashukuru kwamba hakuna ndugu au dada aliyeathiriwa, ingawa wanane wamehamishwa ili kuwaepusha na hatari. Kama 2 Wakorintho 8:14, 15 inavyoonyesha, mizunguko ya karibu imeandaa mahitaji, makao, na usafiri.