NOVEMBA 6, 2024
HISPANIA
Mafuriko Yasababisha Uharibifu Mkubwa Kusini-Mashariki mwa Hispania
Oktoba 29, 2024, mvua kubwa zilinyesha kusini-mashariki mwa Hispania. Maeneo mbalimbali katika mkoa wa Valencia yameripoti kupata mvua kubwa ndani ya saa nane. Kwa kawaida, wanapata kiwango hicho cha mvua ndani ya mwaka mzima. Kwa mfano, mji wa Turis ulipata sentimita 64 hivi za mvua. Mafuriko na maporomoko ya ardhi yalileta matope mengi katika miji mingi na kusababisha uharibifu mkubwa wa barabara na madaraja. Maelfu ya watu bado hawana chakula, maji, na umeme. Watu 217 hivi walikufa na wengine wengi hawajapatikana.
Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata
Kwa kusikitisha, dada mwenye umri wa miaka 77 alikufa
Wahubiri 19 walilazimika kuhama makazi yao
Nyumba 1 iliharibiwa kabisa
Nyumba 21 zilipata uharibifu mkubwa
Nyumba 27 zilipata uharibifu mdogo
Wahubiri 157 walipoteza magari yao katika mafuriko
Majumba 3 ya Ufalme yalipata uharibifu mkubwa
Jitihada za Kutoa Msaada
Wawakilishi wa ofisi ya tawi, waangalizi wa mzunguko, na wazee wa maeneo hayo wanatoa msaada wa kiroho, kihisia, na kimwili
Halmashauri ya Kutoa Msaada inasimamia jitihada za kutoa msaada
Kwa upendo, akina ndugu na dada wanaoishi katika maeneo salama wamewapa makazi ya muda ndugu zao ambao wameathiriwa na mafuriko
Tunahuzunika pamoja na ndugu na dada walioathiriwa na mafuriko hayo nchini Hispania. Tunapata faraja na ujasiri kupitia ahadi ya Biblia kwamba wote wanaomfanya Yehova kuwa nguvu na uwezo wao ‘hawataogopa’ hata katika nyakati za taabu.—Isaya 12:2.