Hamia kwenye habari

NOVEMBA 11, 2014
HONDURAS

Aksidenti Mbaya ya Basi Nchini Honduras

Aksidenti Mbaya ya Basi Nchini Honduras

Asubuhi ya Oktoba 31, 2014, basi lililokuwa likiwasafirisha Mashahidi 57 wa Yehova, ambao walikuwa wamejitolea kuwafundisha Biblia watu wanaoishi Las Flores Lempira, lilipatwa na aksidenti lilipokuwa njiani kutoka San Carlos Choloma. Dereva wa kampuni hiyo ya basi pamoja na Mashahidi 13 waliokuwa katika basi hilo walikufa. Kati ya waliokufa kulikuwa na wasichana wawili wenye umri wa miaka 14 na mwingine mwenye umri wa miaka minane. Mashahidi wale wengine 44 walipelekwa hospitalini kufanyiwa uchunguzi. Wawili kati yao ndio waliohitaji matibabu ya kina lakini tayari wamerudi nyumbani. Mashahidi wengine wanaendelea kuwapa faraja na msaada wanaohitaji. Maziko ya 9 kati ya wale waliokufa katika aksidenti hiyo yalifanywa Novemba 1, 2014, katika eneo la Choloma. Watu 3,000 hivi walihudhuria maziko hayo.

José Castillo, msemaji wa Mashahidi wa Yehova nchini Honduras, alisema hivi: “Tunathamini sana jinsi ambavyo wengine katika jamii na katika mashirika mbalimbali wamekuja kuwasaidia wale walioathiriwa na msiba huu.”

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000

Honduras: José Castillo Adriano, simu +504 9998 0895

Mexico: Gamaliel Camarillo, simu +52 555 133 3048