Hamia kwenye habari

AGOSTI 31, 2017
HONG KONG

Kimbunga Hato Kimepiga Hong Kong na Macau

Kimbunga Hato Kimepiga Hong Kong na Macau

Jumatano, Agosti 23, Hato, kimbunga kikubwa kilipiga eneo la kusini la China, kutia ndani majiji ya Hong Kong na Macau. Hakuna vifo vilivyoripotiwa huko Hong Kong, lakini watu 34 waliumia. Jijini Macau, watu 9 hivi walikufa na watu 153 walijeruhiwa.

Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova jijini Hong Kong, ambayo inasimamia kazi jijini Macau, iliripoti kwamba hakuna Mashahidi waliouawa na kimbunga hicho. Hata hivyo, wengi hawana umeme na maji katika eneo la Macau. Ofisi ya tawi inawasiliana na Mashahidi katika eneo hilo ili kuandaa msaada wa maji ya kunywa na mahitaji mengine kwa waabudu wenzao.

Mashahidi wa Yehova zaidi ya 5,500 wanaishi Hong Kong, na wengine 320 wanaishi eneo la Macau.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000

Hong Kong: Danny Steensen, simu +852-3950-3500