Hamia kwenye habari

NOVEMBA 28, 2018
INDIA

Dhoruba Gaja Yapiga India

Dhoruba Gaja Yapiga India

Novemba 16, 2018, Dhoruba Gaja ilipiga jimbo la kusini la Tamil Nadu nchini India. Watu 46 hivi waliuawa, watu 250,000 walilazimika kuhama nyumba zao, na nyumba zaidi ya 85,000 zimeharibiwa kwa kiwango fulani au kabisa.

Nyumba ya ndugu mmoja katika eneo la Mannargudi, Tamil Nadu, ambayo iliharibiwa na mti ulioanguka.

Ofisi ya tawi ya India imeripoti kwamba hakuna ndugu au dada aliyepata majeraha au kufa kwa sababu ya dhoruba hiyo. Hata hivyo, nyumba 38 za ndugu zetu na pia majumba 2 ya Ufalme yameharibiwa. Ofisi ya tawi ilianzisha Halmashauri ya Kutoa Msaada ili kupanga jinsi msaada utakavyotolewa, msaada unatia ndani kusambaza chakula na maji kwa ndugu walioathiriwa.

Tunasali kwamba ndugu na dada zetu nchini India walioathiriwa na Dhoruba Gaja wapate faraja kutoka kwa Yehova kupitia wazee wanaowachunga kwa upendo.—1 Petro 5:2.