Hamia kwenye habari

Daniel Hutabarat na Wilhinson Sihotang wakiwa mbele ya Jumba la Ufalme huko Batam, katika Visiwa vya Riau

FEBRUARI 26, 2020
INDONESIA

Baraza la Mkoa la Elimu Laheshimu Imani ya Kidini ya Mashahidi Wawili Matineja

Baraza la Mkoa la Elimu Laheshimu Imani ya Kidini ya Mashahidi Wawili Matineja

Januari 22, 2020, Baraza la Mkoa la Elimu nchini Indonesia liliagiza kwamba Mashahidi wa Yehova wawili matineja, Daniel Hutabarat na Wilhinson Sihotang, warudishwe shuleni haraka iwezekanavyo. Ndugu hao wawili vijana walifukuzwa shuleni tangu Novemba 29, 2019, kwa sababu ya kukataa kusalimu bendera na kuimba wimbo wa taifa kwa sababu ya imani yao ya kidini. Januari 23, 2020, walirudi shuleni.

Baada ya kuchanganua hali yao, Baraza la Mkoa la Elimu ilifikia mkataa kwamba ndugu zetu waliheshimu mamlaka za shule na serikali ya nchi. Hawakutaka tu kushiriki katika shughuli yoyote ambayo ingepingana na mambo waliyojifunza kutoka kwenye Biblia. Ndugu Yoga Sulistiono, ambaye anaratibu shughuli za Dawati la Habari za Umma nchini Indonesia anasema hivi: “Mashahidi wa Yehova nchini Indonesia wanafurahia uamuzi mzuri uliofanywa na wanawashukuru wenye mamlaka walioheshimu uhuru wetu wa kidini.”

Zaidi ya yote tunamshukuru Yehova, Mfundishaji wetu Mkuu, kwa uamuzi huu mzuri uliofanywa.—Isaya 30:20.