Hamia kwenye habari

DESEMBA 12, 2016
INDONESIA

Tetemeko Kubwa la Nchi Indonesia

Tetemeko Kubwa la Nchi Indonesia

Mapema Jumatano asubuhi, Desemba 7, tetemeko la nchi lenye kipimo cha 6.5 lilitokea kwenye ufuo wa kaskazini wa kisiwa cha Indonesia cha Sumatra. Zaidi ya watu 100 wamekufa na mamia ya watu wamejeruhiwa.

Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova ya Jakarta ilieleza kwamba wamewasiliana na waamini wenzao wote na hakuna aliyekufa au kujeruhiwa wakati wa tetemeko hilo. Kwa kuongezea, hakuna nyumba au majengo yoyote ya ibada ya Mashahidi yaliyoharibiwa.

Mashahidi wa eneo hilo wanafanya jitihada za pekee kuwafariji na kuwasaidia majirani zao walioathiriwa na msiba huo.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000

Indonesia: Tom Van Leemputten, +62-813-4527-1974