Matukio Muhimu Kihistoria Nchini Israel
MEI 1, 2015—Mahakama Kuu yatoa uamuzi kwamba Mashahidi wa Yehova wana haki ya kukutanika katika jiji la Ra’anana
FEBRUARI 5, 2007—Kwa msaada wa mwanasheria mkuu, mahakama yaamua kwamba Haifa International Congress Center iliwabagua Mashahidi kwa kukataa wakodi jengo lao
Mwishoni mwa miaka ya 1990—Wanaharakati wa dini ya Kiyahudi wazidisha mashambulizi na mnyanyaso dhidi ya Mashahidi
SEPTEMBA 7, 1992—Baada ya tangazo la mwanasheria mkuu, Baraza la Rufaa la Wilaya labadili uamuzi wake na kuwaruhusu Mashahidi watumie tena Jumba lao la Ufalme jiijini Tel Aviv
NOVEMBA 15, 1963—Serikali yasajili shirika la kisheria la Watch Tower Bible & Tract Society
JANUARI 1, 1963—Mashahidi wafungua ofisi ya tawi jijini Haifa, baadaye ilihamishiwa jijini Tel Aviv
1920—Wakati wa mamlaka ya Uingereza katika Mashariki ya Kati, Mashahidi wa Yehova walianzisha kutaniko lao la kwanza na kufungua ofisi ili isimamie kazi yao