Hamia kwenye habari

Moto wa msituni ukiwaka katika kisiwa cha Sicily, Italia. Picha ndogo: Mawe makubwa ya barafu yaliyotokana na mvua ya mawe kaskazini mwa Italia

AGOSTI 4, 2023
ITALIA

Hali Mbaya ya Hewa Kaskazini Mwa Italia na Kwenye Kisiwa cha Sicily

Hali Mbaya ya Hewa Kaskazini Mwa Italia na Kwenye Kisiwa cha Sicily

Kuanzia Julai 22 hadi 26, 2023, Italia ilipatwa na majanga mawili tofauti yaliyosababishwa na hali mbaya ya hewa. Kaskazini mwa Italia, mvua kubwa ilinyesha na kusababisha upepo mkali uliovuma kwa kasi ya zaidi ya kilomita 120 kwa saa. Pia, kulikuwa na mvua ya mawe yenye upana wa sentimita 19. Wakati huohuo, moto uliwaka misituni katika sehemu 330 na kuharibu sehemu kubwa ya kisiwa cha Sicily. Kwa kuwa kiwango cha joto kilifika nyuzi 47 Selsiasi katika eneo hilo basi moto huo ulisambaa kwa kasi zaidi. Matokeo ni kwamba majengo mengi yameharibiwa na mamia ya watu wameachwa bila umeme. Maelfu ya watu wamelazimika kuhama makao yao. Watu watano walikufa.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

Mvua na Mawe na Upepo Kaskazini mwa Italia

  • Hakuna ndugu au dada aliyekufa

  • Ndugu 2 wamejeruhiwa

  • Nyumba 36 zimepata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 242 zimepata uharibifu mdogo

  • Jumba 1 la Ufalme limepata uharibifu mkubwa

  • Majumba 12 ya Ufalme yamepata uharibifu mdogo

Moto wa Msituni Kwenye Kisiwa cha Sicily

  • Kwa kusikitisha, mume na mke walipoteza uhai wao moto ulipozingira nyumba yao

  • Ndugu na dada 48 wamelazimika kuhama makao yao

  • Majumba ya Ufalme na majengo mengine ya kitheokrasi hayakupata uharibifu wowote

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Waangalizi wa mzunguko wanashirikiana na wazee wa makutaniko wa maeneo hayo ili kuandaa msaada wa kiroho na wa kimwili kwa ajili ya wale walioathiriwa na moto katika kisiwa cha Sicily na wale walioathiriwa na mvua ya mawe kaskazini mwa Italia

  • Halmashauri 1 ya Kutoa Msaada ilianzishwa ili kusimamia kazi ya kutoa msaada katika kisiwa cha Sicily

Tunasikitishwa sana na kifo cha ndugu na dada yetu huko Sicily na tunasali kwa ajili ya wote walioathiriwa na majanga haya. Tunatazamia kwa hamu Yehova atakapoondoa matatizo yote hivi karibuni.​—Ufunuo 21:4.