MEI 24, 2023
ITALIA
Mafuriko Yasababisha Madhara Italia Kaskazini
Mvua kubwa zimesababisha mafuriko makubwa katika eneo la Emilia-Romagna lililoko Italia Kaskazini. Kuanzia Mei 15, 2023, eneo hilo lilipata angalau sentimita 50 za mvua katika siku mbili tu. Zaidi ya maeneo katika manispaa 40 ziliathiriwa. Watu 14 wameripotiwa kuwa wamekufa. Maelfu ya watu wamelazimika kuhama nyumba zao.
Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata
Hakuna ndugu au dada yetu ambaye amejeruhiwa au kufa
Wahubiri 342 pamoja na familia zao wamelazimika kuhama makao yao
Nyumba 167 zilijaa maji. Kati ya hizo, nyumba 72 zilipata uharibifu mkubwa
Jumba 1 la Ufalme lilipata uharibifu mkubwa
Majumba 3 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo
Jitihada za Kutoa Msaada
Waangalizi wa mzunguko pamoja na wazee wa eneo hilo wanatoa msaada wa kiroho na wa kimwili unaohitajika sana kwa walioathiriwa
Halmashauri ya Kutoa Msaada imewekwa rasmi ili kusimamia jitihada za kutoa msaada
Tunatarajia kwa hamu wakati ambapo hakuna mtu atakayeogopa misiba ya asili kwa sababu “hema la Mungu [litakuwa] pamoja na wanadamu.”—Ufunuo 21:3, 4.