Hamia kwenye habari

JANUARI 23, 2017
ITALIA

Poromoko Hatari la Theluji Latokea Eneo la Katikati ya Italia

Poromoko Hatari la Theluji Latokea Eneo la Katikati ya Italia

Jumatano, Januari 18, 2017, poromoko kubwa la theluji lilitokea katika eneo la Abruzzo lililoko katikati ya nchi Italia na kufunika kabisa hoteli moja iliyokuwa na watu 30 hivi ndani. Eneo hilo lilikumbwa na tetemeko kubwa la nchi mwezi wa Agosti mwaka uliopita. Poromoko hilo lilitokea baada tu ya matetemeko manne makubwa ya nchi kutokea siku hiyohiyo. Matetemeko hayo yalikuwa na kipimo cha 5.0. Juhudi za kuokoa uhai zinazuiwa na theluji iliyokuwa imeanguka juma lililotangulia, na miji kadha haina umeme na iko katika maeneo ya mbali.

Ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Italia inaripoti kwamba ingawa hakuna Mashahidi walioripotiwa kuwa wamekufa au kujeruhiwa vibaya, wanajaribu kuwasiliana na familia za Mashahidi katika eneo lililoathiriwa zaidi na matetemeko hayo na ambako theluji nyingi ilikuwa imemwagika. Wazee wa makutaniko ya Mashahidi katika eneo hilo wamekuwa wakihakikisha familia hizo zinapata chakula, maji, kuni, na mambo mengine ya lazima. Ofisi ya tawi inaendelea kuangalia hali na kutoa msaada wa ziada unapohitajika.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000

Italia: Christian Di Blasio, +39-06-872941