Hamia kwenye habari

AGOSTI 24, 2017
ITALIA

Tetemeko la Ardhi Latokea Kwenye Kisiwa cha Italia

Tetemeko la Ardhi Latokea Kwenye Kisiwa cha Italia

Agosti 22, tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 4.0 lilitokea katika kisiwa cha Ischia karibu na ufuo wa Naples, Italia. Liliharibu majengo mengi na kuwaacha watu 2,600 hivi bila makao. Zaidi ya watu 40 walijeruhiwa na 2 wakafa.

Hakuna ripoti yoyote inayoonyesha kwamba yeyote kati ya Mashahidi 633 wa Yehova wanaoishi katika kisiwa hicho alijeruhiwa au kufa, lakini nyumba za familia 9 za Mashahidi ziliharibiwa. Mashahidi wa eneo hilo wanatoa msaada na kuwafariji kiroho Mashahidi wenzao walioathiriwa.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000

Italia: Christian Di Blasio, simu +39-06-872941