Hamia kwenye habari

Italia

 

2019-10-10

ITALIA

Uzinduzi wa Jiwe la Msingi la Kumbukumbu ya Mashahidi wa Yehova Walioteswa na Wanazi na Wafashisti Nchini Italia

Tukio hilo lilifanyika huko Risiera di San Sabba in Trieste, Italia, ili kuwakumbuka maelfu ya Mashahidi wa Yehova walioteswa na Wanazi kotekote barani Ulaya.

2019-08-01

ITALIA

Mahakama Kuu ya Italia Yalinda Haki ya Mashahidi wa Yehova ya Kupata Matibabu

Uamuzi uliofanywa hivi majuzi umekazia haki ya ndugu zetu ya kujiamulia wenyewe juu ya matibabu wanayotaka.

2019-07-11

ITALIA

Madaktari Katika Makongamano Mawili Makubwa ya Kitiba Nchini Italia Wapendezwa na Matibabu Yasiyohusisha Damu

Matukio hayo mawili yaliandaa fursa za kutoa habari za karibuni zaidi za matibabu yasiyohusisha damu kwa wataalamu wa kitiba. Pia, baadhi ya madaktari wa upasuaji na wa nusu-kaputi walieleza maoni yao kuhusu kushughulika na Mashahidi wa Yehova.

2018-09-06

ITALIA

Mahakama Jijini Sicily Yathibitisha Haki ya Kujiamulia ya Wagonjwa Mashahidi wa Yehova

Huo ni uamuzi wa kwanza katika mahakama ya Italia ambao umemhukumu daktari kwa uhalifu kwa sababu ya kuvunja haki ya msingi ya mgonjwa kuamua jinsi mwili wake utakavyotibiwa kupatana na imani yake.

2018-06-11

ITALIA

Chuo Kikuu cha Padua Kimefanya Kongamano la Kihistoria la Kuzungumzia Maendeleo ya Matibabu Yasiyohusisha Damu

Kwa muda fulani, ilionekana kwamba kumtia mgonjwa damu mishipani hakuna madhara yoyote na ndiyo mbinu inayoweza kuokoa uhai wakati wa matatizo makubwa ya kiafya au wakati wa upasuaji tata. Lakini wasemaji wengi katika kongamano hilo walipinga wazo hilo.

2018-06-11

ITALIA

Mahojiano na Daktari Luca P. Weltert.

“Watu hawatiwi damu sana mishipani, na si wagonjwa Mashahidi tu, bali wagonjwa ulimwenguni pote, kwa sababu uthibitisho unaonyesha kwamba kutotia damu kunakuwa na matokeo mazuri zaidi.”

2018-06-11

ITALIA

Mahojiano na Profesa Antonio D. Pinna.

“Kwa kweli, sidhani daktari anapaswa kumtendea mgonjwa kwa njia tofauti kwa msingi wa dini. Kwa mfano, kuna wagonjwa ambao si Mashahidi wa Yehova na bado hawataki kutiwa damu mishipani.”

2018-06-11

ITALIA

Mahojiano na Profesa Massimo P. Franchi

“Ninathamini kwamba nimekutana na Mashahidi wa Yehova katika taaluma yangu. Wamenifanya mimi nikiwa daktari anayetumia mbinu za kawaida za tiba, kuanza kuchunguza uwezekano na umuhimu wa kupunguza matumizi ya damu.”

2017-12-07

ITALIA

Wakimbizi Kwenye Kambi Kubwa Zaidi Barani Ulaya Wakaribishwa na Mashahidi wa Yehova

Maofisa katika kambi kubwa zaidi barani Ulaya wanatambua kazi ya Mashahidi wa Yehova ya kuwasaidia wakimbizi wanufaike kutokana na elimu ya Biblia.

2016-12-19

ITALIA

Kisehemu: Mahojiano na Ofisa wa Gereza la Bollate

Jumba la Ufalme la Mashahidi wa Yehova limewasaidiaje wafungwa kuwa na maisha bora?

2016-12-19

ITALIA

Maofisa Nchini Italia Watoa Eneo kwa Ajili ya “Jumba la Ufalme” Ndani ya Gereza kwa Manufaa ya Wafungwa

Maamuzi hayo yalifanywa kutokana na matokeo mazuri ya elimu ya Biblia ambayo imetolewa na Mashahidi kwa wafungwa wa gereza la Bollate kwa miaka 13.

2016-11-08

ITALIA

Kampeni ya Mashahidi Yatoa Faraja Baada ya Tetemeko la Nchi Lililotokea Italia

Mashahidi wa Yehova nchini Italia wakishiriki kampeni ya ulimwenguni pote, Mashahidi wa Yehova katika Italia wanaongeza jitihada zao za kuwapa ujumbe wa faraja waathiriwa wa tetemeko la nchi katika maeneo ya Lazio, Marche, na Umbria.