Hamia kwenye habari

DESEMBA 21, 2022
JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO

Mafuriko na Maporomoko ya Ardhi Yaikumba Kongo (Kinshasa)

Mafuriko na Maporomoko ya Ardhi Yaikumba Kongo (Kinshasa)

Desemba 13, 2022, mvua kubwa ilisababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini Kongo (Kinshasa). Maeneo mbalimbali yalifurika na majengo yakaporomoka na hivyo kusababisha vifo vya watu wasiopungua 141.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Kwa kusikitisha, ndugu 1 amekufa

  • Mhubiri 1 amejeruhiwa

  • Nyumba 3 zimeharibiwa kabisa

  • Nyumba 3 zimepata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 5 zimepata uharibifu mdogo

  • Jumba 1 la Ufalme limepata uharibifu mdogo

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Waangalizi wa mzunguko pamoja na wazee wa makutaniko wanafanya ziara za uchungaji na kuwapa wahubiri walioathiriwa na msiba huo msaada unaohitajika

  • Halmashauri 3 za Kutoa Msaada zilianzishwa ili kusimamia jitihada za kutoa msaada

  • Jitihada zote za kutoa msaada zinafanywa kulingana na miongozo ya usalama ya kujilinda dhidi ya COVID-19

Tunatazamia kwa hamu wakati ambapo Yesu atadhibiti kabisa hali ya hewa duniani na kufanya hali ziwe shwari kabisa kwa dunia na wanadamu.​—Mathayo 8:25-27.