Hamia kwenye habari

Mlipuko wa Mlima Nyiragongo

MEI 31, 2021
JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO

Mlipuko wa Volkano Waharibu Goma, Wengi Wakosa Makao

Mlipuko wa Volkano Waharibu Goma, Wengi Wakosa Makao

Mahali

Goma, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo

Janga

  • Jumamosi ya Mei 22, 2021, Mlima Nyiragongo ulilipuka Kaskazini mwa mkoa wa Kivu, ambayo iko karibu na jiji la Goma, jambo ambalo lilisababisha wengi wakimbie eneo hilo

Athari ambazo ndugu na dada zetu wamepata

  • Wahubiri 2,000 walihamia miji mingine iliyo karibu

  • Watumishi 35 wa wakati wote walikosa makao kwa muda

Uharibifu wa Mali

  • Karibu nyumba 29 za ndugu zetu ziliharibiwa

Jitihada za kutoa msaada

  • Halmashauri ya Kutoa Msaada (DRC) iliandaliwa ili kuandaa msaada. Halmashauri hiyo inashirikiana na waangalizi wa mzunguko na wazee katika maeneo hayo ili kuchunguza uharibifu uliofanyika na kuwapa ndugu na dada msaada wanaohitaji

  • Jitihada zote za kutoa misaada huratibiwa kwa kuzingatia miongozo ya kujilinda na COVID-19

Licha ya kwamba ndugu na dada zetu wengi wamepoteza makao yao, tunafurahi kwamba hakuna yeyote kati yao aliyeathiriwa na janga hili la asili. Tunaendelea kusali kwa ajili yao wanapoendelea kumtegemea Yehova katika kipindi hiki cha taabu.—Nahumu 1:7.

Lava ya moto ikimiminika na kusababisha uharibifu mkubwa kwenye jiji lililo karibu na mlima huo