Hamia kwenye habari

Picha ya angani ya eneo lote la ujenzi, jengo la ofisi linaonekana upande wa juu kulia, na majengo manne ya makazi yanaonekana upande wa chini wa picha.

MACHI 22, 2019
KAMERUN

Habari za Karibuni: Ujenzi wa Ofisi ya Tawi ya Kamerun Unakaribia Mwisho

Habari za Karibuni: Ujenzi wa Ofisi ya Tawi ya Kamerun Unakaribia Mwisho

Ujenzi wa ofisi mpya ya tawi umekuwa ukiendelea nchini Kamerun kwa mwaka mmoja sasa. Kama inavyoonekana katika picha iliyo hapo juu, majengo manne ya makazi pamoja na jengo la ofisi yameshaanza kujengwa. Watu 60 wataweza kuishi hapo na kutakuwa na nafasi 71 za watu kufanya kazi za ofisi. Inakadiriwa kwamba majengo hayo huenda yakaanza kutumiwa mwishoni mwa mwezi wa Desemba 2019. Picha zifuatazo zinaonyesha maendeleo ya ujenzi huo.

Mchoro wa ofisi ya tawi

Julai 2018: Upande wa mbele unaonyesha mstari wa kwanza wa matofali ya ukuta ukiwa umewekwa kwenye Makazi 3.

Agosti 2018: Huu ni msingi wa ukuta utakaojengwa kuzunguka eneo zima.

Septemba 2018: Sehemu ya mbele ya picha inaonyesha Makazi 4, na sehemu yake ya chini imekamilika.

Oktoba 2018: Sehemu hii itakuwa mwingilio mkuu wa eneo la mapokezi katika jengo la ofisi.

Desemba  2018: Majengo ya Makazi 2 na 3 yakiwekewa paa ya chuma.